SERIKALI YAJA NA MIKAKATI MADHUBUTI, UPATIKANAJI WA MBOLEA

Na Deborah Munisi, Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imejipanga kuja na mkakati wa kudumu wa kuhakikisha Wakulima wanapata mbolea ya Ndungu pasi na kutembea umbali mrefu.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Antony Mavunde Leo April 11,2023 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Same Mhe. Anne Malecela alilotaka kujua mkakati wa serikali katika kutatua adha ya umbali wa upatikanaji wa mbolea ya ruzuku, alilouliza kuwa Je? Serikali inampango gani wa uhakika kwa kipindi kijacho kupeleka Mbolea ikiwemo Mbolea ya Ndungu kwa wakulima sehemu zote Jimboni.

Mhe. Mavunde amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo awali na kuahidi kuwepo kwa mikakati madhubuti na tayari serikali imeshachukua hatua ikiwa ni pamoja na Kuwaagiza TFRA kwa kusajili vituo vya mawakala karibu na wakulima, na kutumia Vyama vya Ushirika na kutumia Maghala ya Serikali ili kufikia maeneo ya uzalishaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *