DITOPILE AUNGANA NA WANA MPWAPWA KWA IFTAR, WAMUOMBEA DUA RAIS SAMIA

Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile ameungana na Waumini Mbalimbali katika Msikiti Mkuu wa Mpwapwa Mjini Mkoani Dodoma katika Iftari na Dua Maalum ya kuiombea Nchi na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kabla ya Dua hiyo Mhe. Mbunge alitembelea Gereza Kuu la Mpwapwa na kuwapelekea Wafungwa sadaka ya Futari na mahitaji mbalimbali.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile anaendelea kuwatakia Waislamu wote nchini Ramadhani njema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *