MBUNGE NGASSA: “VIJANA TUTUMIE FURSA ZA ASILI ZILIZOPO KWENYE KATA ZETU”

“Vijana wenzagu nimerudi Jimboni kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri yetu, nilipokuwa naelekea Halmashauri Viongozi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya wakaniambia kuna semina ya mafunzo ya Uongozi kwenu Viongozi wa Vijana wa Kata zote za Wilaya ya Igunga, nimeona nije kuwasalimia ndugu zangu”

“Nimepata nafasi kutoa neno la hamasa kwenu, ushauri wangu kwenu Jumuiya ya Vijana (UVCCM) Wilaya ya Igunga, katika mikakati ya kujiimarisha kiuchumi mnayoiweka, mtumie fursa za asili zilizopo kwenye Kata zenu, tuache mambo ya kuigizana (copy and paste). Fursa za Bukoko hazifanani na fursa za Igurubi, fursa za Mwamashiga hazifanani na fursa za Igunga Mjini. Tubainishe fursa za maeneo yetu ili zitusaidie kuwaza nje boksi na kupambana kujenga uchumi wa Jumuiya yetu (UVCCM) na uchumi wa kila mmoja wetu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *