NAIBU WAZIRI MHE.HAMIS MWINJUMA AIPONGEZA FOUNTAIN GATE KWA KUENDELEZA USHINDI AFRIKA KUSINI

Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma akiwa pamoja na mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ghana Asamoah Gyan wakifuatilia Mashindano ya Fainali za shule za Afrika yaliyoandaliwa na chama cha mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) yanayofanyika Durbun, Afrika Kusini ambapo Tanzania inawakilishwa na timu ya shule ya wasichana ya Fountain Gate.

Fountain Gate wametupa karata yao ya pili leo April 6, 2023 na timu ya shule ya Scan Aid kutoka Gambia ambapo wameibuka na ushindi wa Goli 2 kwa 0 na hivyo kuongoza kundi A kwa jumla ya point 6 hivyo kwenda moja kwa moja kwenye nusu Fainali ya mashindano hayo.

Na mara baada ya mchezo Mhe. Aliwapongeza wachezaji wa timu ya wasichana ya Fountain Gate kwa ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Scan Aid ya Gambia. Katika mchezo wa kwanza Fountain Gate iliibuka na ushindi wa goli 7 kwa moja dhidi ya ya Edendale High School ya Afrika Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *