MBUNGE JESCA MSAMBATAVANGU AITAKA SERIKALI KUTAFUTA MWAROBAINI WA MAPENZI YA JINSIA MOJA.

Na Deborah Munisi, Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mhe. Jesca Msambatavangu ameitaka serikali kuendelea kudumisha na kuimarisha maadili ya Kitanzania kwa Mustakabali wa vizazi vijavyo ikiwemo kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto na kupinga Mapenzi ya jinsia moja.


Ameyasema hayo leo April 6, 2023 Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia kuhusu Hotuba ya Waziri Mkuu juu ya Mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na Makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2023/2024.


Amesema Taifa linawekeza kwa mustakabali wa vizazi vijavyo hivyo, ipo haja ya kuwekwa umakini pasi na kukopa mila na desturi za mataifa ya Nje ambayo yapo kinyume na maadili ya Kitanzania na badala yake Tanania iwe mfano wa kuigwa kwenye maadili.

“Yapo mambo yanayoendelea katika jamii yetu, Tusipokuwa makini na tukienda kwa kukopi na kupaste kwasababu mataifa fulani yamesema, ipo wakati sisi kama watanzania tutoe fursa kwa mataifa mengine yaje yajifunze kutoka kwetu, yaje yajifunze kutoka kwetu namna ambavyo tunalea na kuwakuza watoto wetu, waje waone namna ambavyo waafrika inatunza watoto wake” Amesema Mhe. Msambatavangu


“Swala hili linalohusiana na ukatili kwa watoto wetu, ulawiti na ubakaji kwa watoto wetu na maswala ya ndoa ya jinsia moja yasifumbiwe macho,tuyaongelee makanisani,Misikitini, tunaanza hapa bungeni tuyaongelee Serikalini na kwenye Familia zetu, Tutapotea hizi reli zitakuja kupandwa na popo kama ilivyokuwa Sodoma na Domora, huo umeme na majengo makubwa tunayoyajenga hayatakuwa na maana “Amesema Mhe. Msambatavangu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *