MBUNGE ESTHER MATIKO AELEZA KUTORIDHISHWA NA UTEKELEZWAJI BAGETI ZINAZOPITISHWA BUNGENI

Mbunge wa viti maalum Chadema Mhe. Esther Matiko ameeleza kutoridhishwa na utekelezwaji wa bajeti ambazo zinazopitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema hayo Leo April 6, 2023 Bungeni jijini Dodoma wakati wakati akichangia kuhusu Hotuba ya Waziri Mkuu juu ya Mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na Makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2023/2024.


“Fungu namba 65, Tulitenga takribani Bilion 26.6 na tukazielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Wizara ambayo ni muhimu lakini cha kusikitisha mpaka kufikia February mwaka 2023 kulikuwa kumepelekwa Bilion 5.5 tu kama asilimia 22 tu” Alisema Mhe. Matiko.


“Tulitenga Bilioni 3 kwa ajili ya kukarabati na kujenga vyuo vya watu wenye ulemavu kundi ambalo ni maalumu lakini mpaka leo hata senti moja haijawahi kutolewa Piah tulizitenga kwaajili ya kwenda kukuza kazi ya Staha nchini, kukuza uchumi Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uvico 1, Mfuko wa maendeleo ya Vijana, lakini bajeti inatekelezwa kwa asilimia 22 tu” Alisema Mhe. Matiko.


“Nampongeza Rais Samia kwa kuwa muwazi na kukemea uwajibikaji pale aliposema, wale wote ambao walikuwa wanahusika na Ku-invoice hizi ammount waweze kuwajibika, Tungependa waje watueleze mpaka sasa hivi na baada ya hiyo stattement ya Rais, kama bunge lazima tuisimmie Serikali,Watueleze bayana” Alisema Mhe. Matiko
Kufuatia mjadala huo ukamuibua Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba kwa kuwatoa hofu watanzania na kuahidi hatua za kunidhamu kuchukuliwa kwa waliohusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *