MAMA SALMA KIKWETE ALITAKA BUNGE KUTOA AZIMIO LA KUDHIBITI MAPENZI YA JINSIA MOJA

Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi Mhe. Mama Salma Kikwete amewataka wabunge kuwa na Azimio la Kukataa mapenzi ya jinsia Moja kwa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya ukatili kama vile ulawiti.
Ameyasema hayo Leo April 6, 2023 Bungeni jijini Dodoma wakati wakati akichangia kuhusu Hotuba ya Waziri Mkuu juu ya Mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na Makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Amesema unyanyasaji wa Kijinsia kwa watoto, Ndoa za jinsia moja, Malezi na makuzi ya watoto havikubaliki kwenye Jamii ya Kitanzania kwani watoto ndiyo Taifa la Kesho na tegemeo la Taifa kwa kutoa mfano.

“Tufikirie kwamba unamtoto wako umemuacha nyumbani, unaambiwa mtoto huyo ameingia kulawitiwa, kama Mzazi kama Mlezi unajisikiaje? sisi tumepewa dhamana ya kuwalinda, kuwatetea, na kuwasemea” Alisema Mama Salma.


“Kwenye hili ni jambo ambalo hatukubaliani nalo, kama Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kwenye jambo hili tusiletewe vitu kutoka huko, sisi kama watanzania tuna Utamaduni, Mila na Desturi zetu ambazo ndizo zinazotuongoza” Alisema Mama Salma.
Amehitimisha kwa kusema jambo hilo ni la kulaaniwa na ni lazima Wabunge waazimie kwani ndiyo wenye Maamuzi ya kukataa jambo hilo. Alisema Mama Salma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *