WAZIRI MKUU AZIPONGEZA SIMBA SC NA YANGA SC.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amevipongeza vilabu vya Simba na Yanga kutinga hatua ya Robo fainali katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Pongezi hizo amezitoa Leo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hotuba kuhusu Mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na Makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Ametumia nafasi hiyo Kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa motisha kwa vilabu vya ndani vinavyoshiriki mashindano ya Kimataifa kupitia Goli la Mama.

“amekuwa akitoa shilingi milioni tano kwa kila goli linalofungwa, Sote tumeshuhudia Simba Sports Club almaarufu Wekundu wa Msimbazi wakijitwalia kitita cha shilingi milioni 50, wakati huo huo klabu ya Young Africans Sports Club almaarufu Timu ya Wananchi wakijitwalia shilingi milioni 45” Amesema Mhe. Majaliwa

“Ninavipongeza
sana vilabu hivyo kwa kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Ni matumaini yetu sote kuwa vilabu hivyo na vingine vinavyoshiriki mashindano ya kimataifa vitaendelea kujituma na kupambana ili vikombe vya ushindi vije nyumbani” Amesema Mhe. Majaliwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *