SERIKALI KUPITIA OFISI YA WAZIRI MKUU YAOMBA SHILINGI 173,733,110,000 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

Serikali kupitia Ofisi ya waziri MKUU na Taasisi zilizo chini yake imeliomba Bunge kuidhinisha jumla ya shilingi 173,733,110,000; kati ya fedha hizo, shilingi 121,364,753,320 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na shilingi 52,368,356,680 kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.


Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hotuba kuhusu Mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na Makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

“kwa mwaka2023/2024, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake inaliomba Bunge lako Tukufu
liidhinishe jumla ya shilingi 173,733,110,000; kati ya fedha hizo, shilingi 121,364,753,320 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na shilingi 52,368,356,680 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo” Amesema Mhe. Majaliwa

“Mheshimiwa Spika, naliomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 165,627,897,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge, Kati ya fedha hizo, Shilingi 160,458,877,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 5,169,020,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *