SPIKA DKT. TULIA AMPONGEZA RAIS SAMIA, ATOA UTARATIBU WA RIPOTI YA CAG

Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Akson amempongeza Mhe. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri katika eneo la Diplomasia ya Uchumi.

Pongezi hizo amezitoa LeoApril 4 2023, bungeni jijini Dodoma ikiwa ni Bunge la 12 mkutano wa 11 mwaka 2023 baada ya Azimio la bunge la kumpongeza Rais Dkt. Samia kwa kuimarisha Demokrasia nchini na kukuza Diplomasia ya uchumi.

Dkt. Tulia amesema pongezi hizo ni za muhimu hasa kwa Muhimili kama wa bunge kwani ni kazi yao kuishauri na kuisimamia serikali hivyo Mhe. Dkt. Samia anapofanya vizuri ni muhimu kumpongeza kwa lengo la kumtia moyo.

Wakati huo huo ametoa utaratibu wa ripoti ya CAG kwa mujibu wa Sheria na kanuni za katiba huku akitoa onyo kwa vyombo vya habari kutoa taarifa za upotoshaji za bunge.

Amesema ni vyema Vyombo vya habari kuzingatia maadili ya tasnia hiyo kwa kufanya kazi kwa weledi kwani kufanya hivyo wanaibua hisia za upotoshaji wa umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *