
Serikali imeendelea kuchukua hatua endelevu kwa Wakurugenzi katika halmashauri ambao walidhibitika kutosimamia ipasavyo marejesho ya mikopo ya asilimia 10%
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge Viti Maalum Halima Mdee ambalo alilohoji upotevu wa shilingi bilioni 88 za mikopo ya Halmashauri, ni lini serikali itachukua hatua za kisheria kwa wakurugenzi walioshindwa kusimamia marejesho ya fedha za asilimia 10 za mikopo ya wanawake,vijana na Wenye ulemavu.

