MBUNGE OLE SENDEKA-“UKIONA VYAELEA UJUE VIMEUNDWA”

Kama waswahili wasemavyo Chanda Chema huvishwa Pete, Mbunge Christopher Olesendeka ametumia nafasi yake kwa kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kusimama na mabega ya Marais waliomtangulia (awamu) na kuiweka rekodi ya juu katika masuala ya Demokrasia na Diplomasia ikiwa ni pamoja na kuzunguka katika mataifa ya jirani ikiwa ni katika kuongeza mahusiano mema.

Pongezi hizo amezitoa Leo April 4 2023, bungeni jijini Dodoma ikiwa ni Bunge la 12 mkutano wa 11 mwaka 2023 wakati wa kujadili Azimio la bunge la kumpongeza Rais Dkt. Samia kwa kuimarisha Demokrasia nchini na kukuza Diplomasia ya uchumi.
“Kupitia filamu ya Royal Tour tumeshuhudia wawekezaji na wafanyabiashara hapa nchini wakiungana na dunia nzima!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *