MBUNGE MASANJA AGAWA MITUNGI 100 YA GESI KWA WAJASIRIAMALI NA VIFAA VYA MICHEZO KWA SHULE TATU WILAYANI UKEREWE

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja amegawa mitungi ya gesi 100 kwa wanawake wajasiriamali na Vifaa vya Michezo kwa shule tatu Wilayani Ukerewe jana Machi 29, 2023 ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kuwawezesha wajasiriamali na kuunga mkono masuala ya michezo mashuleni Mkoani Mwanza.

Vifaa hivyo vya michezo vilivyokabidhiwa kwa shule za Sekondari za Nansio, Bukongo na Namagondo ni pamoja na mipira na jezi vyenye thamani ya shilingi milioni 3,350,000.

Pia katika ziara hiyo, Mhe. Masanja amekabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 3,000,000 kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali hao kuendelea kujinunulia nishati gesi kwa ajili ya biashara zao.

Awali akizungumza na wanafunzi hao, Mhe. Masanja aliwaasa kusoma kwa bidii,kuwa na hofu ya Mungu , nidhamu na kuwaonya kutojihusisha na mambo ambayo sio utamaduni wa Mtanzania.

Aidha aliwataka wajasiriamali kutumia nishati mbadala na kuachana na matumizi ya nishati chafu ambayo ina athari kwa afya ya binadamu na mazingira kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *