MBUNGE DITOPILE AFUTURISHA DODOMA, WAMUOMBEA DUA RAIS SAMIA.

Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile ameaandaa Iftari na Dua Maalum ya Watoto Yatima na Wajane kuiombea Nchi na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hafla hiyo ya Iftari imefanyika katika Hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma ambapo Mgeni wa Heshima alikua ni Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu ambaye aliambata na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini David Kihenzile.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile anaendelea kuwatakia Waislamu wote nchini Ramadhani njema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *