SAASHISHA CUP YAPAMBA MOTO, MICHEZO MIWILI KUCHEZWA LEO 27-03-2023

Michuano ya Ligi ya Saashisha CUP imeendelea kutimua vumbi kwa Michezo miwili kupigwa katika Viwanja Tofauti ikiwa ni hatua ya ishirini bora huko katika Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro ambapo Kware Fc imeibuka kuwa vinara wa bao 2-1 Dhidi ya Mpinzani wake Kia Fc huku Lambo Fc ikiiichabanga Sadala Fc bao 1-0.


Michuano hiyo iliyoanza kupigwa katika majira ya saa kumi na nusu jioni katika dimba la Half London bao mabao ya Kware Fc yakifungwa na Mchezaji Devid Munisi huku Boa moja la mpizani wake Kia Fc likifungwa na Ezekieli Jujumani na hatimaye dakika tisini za mchezo zikaipatia ushindi Kware Fc Wakati huo huo Mtanange ukiendelea kupigwa katika dimba la Mailisita Timu ya Lambo Fc ikaipa kichapo 1-0 timu ya Sadala Fc bao lililofungwa na Ally Masilo.


Mechi zingine mbili ziitaendelea leo tarehe 27 Machi 2023, zikiikutanisha timu ya Mail Sita Fc dhidi ya Mroma Fc katika uwanja wa Half London huku Mchezo wa pili ni katika dimba la Mail sita ambapo mtanange utakuwa kati ya Orori Fc dhidi ya Lyamungo Fc majira ya jioni.


Ikumbukwe kuwa lengo la Saashisha Cup ni kwa lengo la kukuza vipaji, kuunga mkono juhudi za Chama cha Mapinduzi CCM katika kutengeneza ajira kupitia michezo, Kuimarisha Afya na kuwafanya wananchi wake kuwa na furaha.

Matukio Katika Picha Wakati wa Mtanange wa Kware Fc dhidi ya Kia Fc (Half London), Sadala Fc dhidi ya Lambo Fc (Mailisita).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *