MKURUGENZI MKUU NHC AWAPONGEZA WAHANDISI NA WASIMAMIZI WA MIRADI

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Shirika hilo Jijini Dodoma ili kujionea utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Machi 12, 2023 alipotembelea miradi hiyo. Katika ziara hiyo ametembeleamradi wa Chamwino kunapojengwa nyumba za makazi  pamoja na mradi wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini – GPSA unakotekelezwa ujenzi wa kituo cha mafuta cha mji wa serikali Mtumba.

Bw. Hamad amewasisitiza Wahandisi na Wasimamizi wa miradi hiyo  kufanya kazi kwa weledi mkubwa na ufanisi wa hali ya juu ili kuendeleza taswira nzuri ya Shirika iliyojijengea kwa muda mrefu. 

Aidha, amesema kuwa Shirika la Nyumba laTaifa linalo wajibu wa kuikamilisha miradi hiyo kwa wakati ili majengo hayo yaweze kuisaidia serikali kutekeleza majukumu yake ya kuhudumia wananchi kwa ufanisi mkubwa.

Bw. Hamad ameridhishwa na utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa na viwango vya ujenzi vinavyoendelea na amewapongeza watendaji wote kwa kazi nzuri.

HABARI PICHA MATUKIO MBALIMBALI ZIARA YA MKURUGENZI NHC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *