TIMU ZATOANA JASHO SAASHISHA CUP.

Leo Machi 25, 2023 Michuano ya Saashisha Cup imeendelea kutimua vumbi Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro mnamo majira ya Saa 10:00 Jioni katika Dimba la Halmashauri ya Hai, umeshuhudiwa mchezo mgumu ambao umezikutanisha Timu ya Home Boys dhidi ya Paris ambapo matokeo katika mchezo huo ni kwamba Home Boys wameibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja 2-1 .


Mabao ya Home Boys yametiwa kimiani na mchezaji hatari Bwana Ronald Huku goli la vijana wa Paris likitiwa kimiani na Kijana aitwaye Seperatu.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa ngumu Sana na ya kuvutia katika michuano hii imefanya Dakika tisini kuvutia upande wa vijana wa Home Boys.

Mchezo huo uliochezwa katika majira ya saa 10:00 Jioni ikiwa ni mwendelezo wa Ligi ya Kombe la Saashisha (SAASHISHA CUP) ambayo inadhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Mafuwe.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kutimua Vumbi hapo kesho ambapo nyasi zinatarajiwa kuwaka moto katika viwanja viwili tofauti kwa Michezo miwili itakayopigwa Majira ya Jioni ambapo mchezo wa mapema utaikutanisha Timu ya KIA FC ambao watamenyana na KWARE FC katika Dimba la Half London.

Mchezo wa pili kwa Siku ya kesho ni kati ya Kwa Sadala Fc ambao watatoana jasho na Lambo Fc katika uwanja wa Mailisita.

Lengo la Michuano ya Saaahisha Cup ni katika kuunga mkono juhudi za Chama cha Mapinduzi CCM katika kutengeneza ajira kupitia michezo pamoja na kutengeneza urafiki baina ya watu tofauti, Kuimarisha Afya na kuwafanya kuwa na furaha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *