
Washiriki mbalimbali wa mashindano ya Saashisha CUP leo Machi 23, 2023 wamepokea vifaa vya Michezo kwaajili ya Mashindano hayo ambayo yamefikia hatua ya Robo Fainali.
Ligi hiyo ya Saashisha CUP inaendelea kutimua vumbi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro ambayo yanashirikisha timu kutoka Kata zote 17 za Jimbo la Hai.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya Shilingi Milioni 27 na laki tano vimekebidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Amir Mkalipa pamoja na Katibu wa Mbunge Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Saashisha Mafuwe.
Aidha lengo la mashindano hayo ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuwatumikia Wananchi wake katika kila sekta ikiwemo Mpira wa miguu kwa lengo la kuzalisha ajira, kuinua uchumi na kujenga afya.
Washiriki hao wametakiwa kushiriki kwa furaha na amani wakati wote na huku wasimamizi wakitakiwa kutenda haki.
Mbali na zawadi zitakazoolewa kwa timu zitakazofanya vizuri, ahadi nyingine kwa timu bingwa zitapewa ni kualikwa kutembelea Bungeni jijini Dodoma.
Matukio Katika Picha yakionyesha washiriki wa Saashisha CUP wakipokea vifaa vya Michezo, leo Machi 23, 2023 ambavyo vimekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Amir Mkalipa pamoja na Katibu wa Mbunge Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Saashisha Mafuwe.












