MSCL YAAGIZWA KUTAFUTA MASOKO

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Jerry Silaa akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kukagua mradi wa ukarabati wa MT Sangara inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za meli (MSCL) Mkoani Kigoma.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imemtaka Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kuhakikisha kitengo cha masoko kinaanza kutafuta kampuni za kusafirisha mzigo kwenye meli zinazojengwa na kufanyiwa ukarabati ili kuziwezesha meli hizo kuanza kazi mara moja baada ya ujenzi na ukarabati kukamilika.
Akizungumza mkoani Kigoma mara baada ya kukagua mradi wa ukarabati wa meli ya MT. Sangar ana eneo ambalo litajengwa chelezo kipya Mhe. Jerry Silaa amesema uwekezaji wa fedha uliowekwa hususani kwenye miradi ya ujenzi na ukarabati wa meli unawapa jukumu Kampuni hiyo kuhakikisha wanapata mzigo wa uhakika utakaowawezesha kupata fedha na hatimaye kuanza kujilipa mishahara na kuendesha
kampuni bila kutegemea fedha kutoka Serikalini.

PICHA 3
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Jerry Silaa akishuka kutoka kwenye Meli ya MT. Sangara mara baada kukagua ukarabati wake, Mkoani Kigoma.


“Serikali imeshaweka fedha nyingi kwenye kampuni hii, na kamati yetu ina jukumu la kuhakikisha mnapata fedha za kuweza kujiendesha wenyewe pasipo kutegemea ruzuku kutoka Serikalini, mtafanikiwa kupata fedha mtaanza huduma za kusafirisha mizigo kupitia meli hizi’ amesema Mhe. Silaa.
Mhe. Silaa ameitaka bodi hiyo kumlipa Mkandarasi Kampuni ya KTMI ambayo ndio yenye kandarasi ya kujenga meli hiyo ili kuepuka madeni ambayo yanaweza kuzalishwa kutokana na kucheleweshwa kwa malipo.
Aidha, Mwenyekiti Mhe. Silaa ameipongeza Bodi, Menejimenti na Watumishi wa Kampuni hiyo kwa kusimamia vyema miradi inayotekelezwa na kuhakikisha wahandisi wake wanapata ujuzi ili kuweza kusimamia vyema meli hizo mara baada ya ujenzi na ukarabati kukamilika.

Muonekano wa hatua meli ya MT. Sangara ambayo inakarabtiwa na Kampuni ya KTIMI ya Nchini Korea Kusini kwa gharama ya shilingi takribani bilioni 8 na ukarabati huo umefikia asilimia 90 na unatarajiwa kukamilika mwezi aprili mwaka huu.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya MSCL, Meja Jenerali Mst. John Mbungo amemuhakikishia Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Mhe Silaa kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati na tayari Kampuni imeshaweka mpango wa muda mfupi na mrefu kwa wa namna fedha iliyowekezwa inaweza kurudi kwa kuhakikisha mzigo wa uhakika unapatikana.
Naye Mtendaji Mkuu wa MSCL, Eric Hamis amesema mradi wa ukarabati wa MT. Sangara unatekelezwa na Kampuni ya KTMI kutoka nchini Korea Kusini kwa gharama ya takribani shilingi bilioni 8 na kwa sasa umefikia asilimia 90 na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi April mwaka huu.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya HUduma za Meli (MSCL), Eric Hamiss akimuonesha Mwenyekiti na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) eneo la Katabe lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Chelezo kipya, wakati kamati hiyo ilipokuwa katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na kampuni hiyo, Mkoani Kigoma.


Eric ameongeza kuwa miongoni mwa matokeo ya ukarabati huo mkubwa ni pamoja kupungua kwa masaa ya safari ambapo utaiwezesha meli hiyo kusafirisha mzigo kwa saa 6 tu ukilinganisha na hapo kabla ambapo ilikuwa inatumia saa zaidi ya 15 kwa safari moja.

Kamati ya KUdumu ya Bunge ya Uwekezaji wa MItaji iko Mkoani Kigoma ambapo imepokea taarifa za utendaji wa taasisi za WIzara ya Ujenzi na Uchukuzi na kutembelea miradi inayotekelezwa kwa mwaka 2022/23.

Mhandisi Mkuu kutoka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Abel Gwanafyo akifafanua kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), kuhusu hatua iliyofikiwa ya ukarabati wa meli ya MT. Sangara wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa ukarabati wa meli hiyo, Mkoani Kigoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *