
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson amezindua program maalum ya mikopo kwa Wanawake na Vijana kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) yenye lengo la kukuza na kuimarisha sekta ya Kilimo nchini.
Hafla hiyo imefanyika leo Machi 21, 2023 katika Ukumbi wa Morena Jijini Dodoma huku ikiwahusisha Wadau mbalimbali katika sekta hiyo pamoja na wanufaika.



