PROF. MBARAWA- NI WAJIBU WA VIONGOZI KUBAINI MAPUNGUFU YA WATUMISHI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza jambo kwa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi (hawapo pichani), wakati akifungua baraza hilo, jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amewataka viongozi wa Sekta ya Uchukuzi, Idara na Taasisi zake kubaini mapungufu ya watumishi na kuyafanyia kazi sanjari na kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wasio timiza wajibu wao .
Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa sekta ya Uchukuzi Profesa Mbarawa Amesema viongozi wa idara na taasisi ni wajibu wao kugundua changamoto za watumishi wa sekta na kuwachulia hatua wale wasio timiza wajibu wao.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Sekta ya Uchukuzi, ambaye ni Katibu Mkuu-Uchukuzi, Bw.Gabriel Migire, akizungumza na wajumbe
wa baraza (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanyakazi Sekta ya Uchukuzi, lililofanyika Jijini Dodoma.

“Niwaombe viongozi wote wa sekta ya Uchukuzi na Taasisi zake viongozi wabaini mapungufu yaliyopo kwa watumishi na kufanyia kazi Aidha tusisite kuchukua hatua kwa watumishi wasio timiza wajibu
wao,”
Aidha ametoa rai kwa taaisisi zote zilizopo chini ya sekta ya uchukuzi kuhakikisha zinawashirikisha watumishi wao katika kupitia mipango na bajeti za taasisi kabla ya kuziwasilisha kwa msajili wa hazina.
Kwa hatua nyingine Mbarawa amezitaka taasisi kuwasilisha michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kupunguza usumbufu kwa wastaafu ili kuepuka adhabu za tozo inayotokana na ucheleweshaji wa kuwasilisha michango hiyo.

Baadhi ya Wajumbe wa Sekta ya Uchukuzi, wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (hayupo
pichani) wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanyakazi, lililofanyika Jijini Dodoma.

“Taasisi nyingi za Umma hazitekelezi wajibu huo na kuichafua serikali, hivyo kila taasisi ifanye uhakiki na uchambuzi wa madeni ya watumishi hususan wastaafu na kuainisha mikakati ya kulipa madeni hayo”
Kwa upande wake Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Bwana, Gabriel Migire amesema sekta yake imejipanga kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa na serikali inakamilika kwa wakati.

“nikuhakikishie tunakwenda kuwa wakali ili kuhakikisha miradi yote inatekelezwa na kukamilika kwa wakati hii itasaidia malengo ya serikali kufikiwa kama ilivyopangwa”
Aidha amesema sekta ya uchukuzi kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 inatarajia kutekeleza miradi ya barabara, ujenzi wa Reli ya SGR, bandari, usafiri wa anga, ununuzi wa rada, pamoja na kuboresha vyuo
vya mafunzo katika sekta ya uchukuzi.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia kwa waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa
baraza la wafanyakazi Sekta hiyo, mara baada ya kufungua baraza la Sekta ya Uchukuzi, Jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *