KAMATI YA LAAC YAELEKEZA KUKAMILISHWA KWA BWALO NA BWENI SHULE YA SEKONDARI IDETE – UYUI

OR TAMISEMI

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uyui kutenga fedha za kukamilisha ujenzi wa Bwalo, Bweni la Wasichana katika shule ya Sekondari Idete.

Hayo yameelezwa leo tarehe 18 Machi 2023 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Stanslaus Mabula (Mb) wakati alipoambata na Kamati hiyo kukagua utekelezaji wa Miradi hiyo.

Kamati ya LAAC imejione ujenzi wa Bwalo ukiwa katika hatua za ukamilishaji pamoja na ujenzi wa bweni la Wasichana ukiwa umebakiza kuwekwa vigae, uwekaji wa dari, upakaji wa rangi pamoja na kutokamilishwa kwa vyoo na mifumo yake.

Aidha, Mhe. Mabula amemtaka mkurugenzi kuchukua hatua za haraka kwa kukamilisha vyoo na kujenga mfumo wa maji taka katika bweni la wasichana ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi kufuata vyoo mbali na bweni.

Mhe. Mabula ameagiza kufanywa kwa marekebisho ya mfumo wa umeme kwenye madarasa mawili na kutengeneza eneo la kupita wakati wa dharura, kabla ya tarehe 25 Machi 2023 kulingana na BOQ.

Mhe. Mabula amesema Halmshauri ihakikishe miradi yote ambayo haijakamilishwa iwekewe mpango wa kukamillihwa ili ilete tija na kuanza kutoa huduma.

Katika mwaka wa fedha 2020/21 Serikali ilitoa Milioni 100 kujenga bwalo la chakula, Shilingi milioni 80 kujenga bweni la wasichana, milioni 40 kujenga madarasa mawili na milioni 6 na laki 6 kujenga matundu 6 ya vyoo katika shule ya sekondari Idete.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *