Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ilala Bw. Mtiti Jirabi ameagiza uongozi Kata na Matawi kuitisha vikoa na kuzungumza na wananchi kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu matukio ukatilia wa kijinsia yanaendelea ikiwemo ubakaji na ulawiti, jambo ambalo litasaidia kuondokana na matukio hayo.
Akizungumza leo Machi 17, 2023 Jijini la Dar es Salaam kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mhe. Mohamed Msofe, Katibu wa Jumuiya hiyo. Bw. Mtiti Jirabi, amesema kuwa kupeleka elimu kwa wazazi ya kupinga matukio uhalifu na mmong’onyoko wa maadili itasaidia kuwa fundisho kwa watu wenye tabia hizo.

“Nasisitiza mtu yoyote atakayebainika anafanya vitendo vya ukatilia kwa watoto tutamchukuliwa hatua kali za kisheria” amesema Bw. Jirabi.
Amebainisha kuwa katika Shule hiyo kuna baadhi ya wanafunzi wanafanyiwa vitendo vya ukatilia ikiwemo ubakaji katika maeneo wanapoishi jambo ambao sio rafiki kwa maendeleo yao.
“Tumechukua changamoto zote za Shule, tunakwenda kuzipeleka ili zifanyiwe kazi kwa ukaribu, Jumuiya ya wazazi CCM ipo karibu na uongozi wa Shule katika kuhakikisha tunashirikiana kutatua matatizo yote” amesema Bw. Jirabi.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji, Jumuiya ya Wazazi Chama Cha CCM Wilaya ya Ilala, Bw. Abdallah Othman, amesema kuwa mazingira ya Shule imezungukwa na watu wanaofanya matendo maovu ikiwemo kuvuta bangi jambo ambalo linapelekea baadhi ya wanafunzi kujiingiza katika makundi hayo.

“Nyuma ya shule hii kuna mateja na Shule haina uzio, hivyo kama Jumuiya ya wazazi tumeichukua changamoto hiyo na tunaipeleka sehemu husika, Shule ikiwa na uzio itasaidia kujenga nidhamu kwa wanafunzi” Bw. Othman
Mkuu wa Shule ya Sekondari M chikichini Bw. Nelson Nestory ameipongeza kamati ya Jumuia ya Wazazi CCM kwa kufika kwa ajili kujua changamoto za wanafunzi na walimu, huku akieleza kuwa wamejifunza mambo mengi kutoka kwao.
Bw. Nestory amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo ni ukosefu wa uzio katika Shule hiyo ambapo inachangia wanafunzi kukosa uhuru wa kuzunguka katika eneo la Shule.
“Nyuma ya Shule hii kuna mateja, na wakati mwengine wanawanyang’anya chakula wanafunzi, hivyo tunaomba wadau mbalimbali wajenge uzio ili kuwawasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki zaidi” amesema Bw. Nestory.
Mkuu huyo wa Shule amewataka wazazi waoneshe ushirikiano katika uwalea watoto, kwani kuna changamoto ambazo zinaitaji ushirikiano wao ili kuzitatua.
Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala kupitia Kamati ya Utekelezaji Wazazi Wilaya imeendelea na ziara yake kupita kwenye Shule za Msingi na Secondari, ambapo leo Mach 17, 2023 imefika Shule ya Secondary ya Mchikichini na kukutana na Wanafunzi na kufanya Kikao kazi na Bodi ya Shule hiyo.
