WADAU WA ULINZI NA USALAMA WALISHUKURU JESHI LA POLISI KWA KUTOA VIFAA MBALIMBALI

Na mwandishi wetu Jeshi la Polisi

Wadau wa Ulinzi na usalama wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama hapa Nchi ambapo waliomba Jeshi hilo kuendelea kudhibiti uhalifu ili kuendeleza sifa nzuri ya Tanzania ambayo inasifika kwa tunu ya amani na utulivu.

Kauli hiyo imetolewa leo march 17 2023 na mwakilishi wa kampuni ya Puma Kutoka Temeke jijini Dar es salaam Bwana Muslim Baruan wakati akitoa vifaa mbalimbali vya michezo katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam ambapo amebainisha kuwa wao kama wananchi wanajivunia kuwa na Jeshi ambalo linajua wajibu wake katika kulinda Rai na mali zake.

Ameongeza kuwa wananchi wameendelea kufanya kazi zao kwa amani kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Jeshi hilo ambapo amebainisha kuwa wamepatakumsukumo huo kutokana na askari hao wanavyo fanya mazoezi yao ya kila siku nyakati tofauti tofauti ikiwemo nyakati za usiku.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Daktari SACP LAZARO MAMBOSA amesema kitendo cha kutoa vifaa hivyo sit u kuongeza vifaa bali wameongeza usalama wa askari wakati wa mazoezi ambapo amebainisha kuwawadau hao wa maswali ya ulinzi wamefanya jambo jema kuongeza vifaa hivyo vya mazoezi.

Daktari Mambosasa amesema vifaa hivyo vitakwenda kutumika vyema kwa ajili ya kulinda Maisha ya askari wanapokuwa katika mazoezi nyakati za usiku ambapo amesema kuwa mtaji wao mkubwa katika kozi mbalimbali za kijeshi ni utimamu katika afya ya askari ili aweze kudumu mafunzo yanayotolewa.

Sambamba na hilo ameipongeza kampuni hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kushiriki kikamilifu katika maswala ya ulinzi na usalama na kuwaomba kuendelea na moyo huo huo wa kushirikiana na Jeshi la Polisi na setikli kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *