KAIRUKI AZUNGUMZA NA WABUNGE KUTOKA MKOA WA SHINYANGA.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wabunge katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao hasa katika sekta ya afyamsingi, elimumsingi na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 3 Februari, 2023 jijini Dodoma alipokutana na wabunge wa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.

Amesema Serikali itaendekea kuhakikisha wananchi wanaoelekewa maenedele na kuimarisha mazingira wezeshi katika sekta ya elimu, afya na barabara.
Katika kikao hicho, wabunge kutoka Mkoa wa Shinyanga wameishukuru Serikali kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Waziri Kairuki ameweka utaratibu wa kukutana na Wabunge wa Majimbo ambapo mpaka sasa amekutana na wabunge wa Mikoa ya Mbeya, Dodoma, Mwanza, Dar-es salaam, Tanga, Kilimanjaro, Mara, Dodoma, Shinyanga, Kagera na Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *