WAKUU WAVIKOSI VYA KIJESHI WATAKIWA KUSIMAMIA MAENEO WALIYOPEWA DHAMANA YA KULINDA KISHERIA

Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Innocent Bashungwa amewataka Wakuu wa vikosi,shule na vyuo vya kijeshi kusimamia maeneo waliyopewa dhamana ya kuyalinda kisheria.

Waziri Bashungwa amesema hayo wakati akifungua mkutano wa Sita wa Mkuu wa Majeshi na Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Unaofanyika Mjini Songea Mkoa wa Ruvuma ambapo amesema jeshi lipo kwenye utaratibu wa kupitia upya na kupima maeneo yake dhidi ya wavamizi wa maeneo ya jeshi ambayo yamekuwa yakileta mgogoro kwa jamii inayoyazunguka.

“Maeneo yote ya jeshi nchini yapate hati miliki ili kuwe na legal force dhidi ya uvamizi unaoendelea maeneo mbalimbali ya vikosi vyetu kwahiyo vikosi na vyuo wawaelimishe maafisa na askari kuhusu kuacha kuvamia maeneo ya jeshi” Waziri Bashungwa.

Katika Hatua nyingine Waziri Bashungwa amesema jeshi la Tanzania linaendelea kuaniwa kimataifa kutokana na kuendelea kufanya vizuri katika operesheni za Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wake mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda amesema jeshi hilo linaendelea kutoa mafunzo kwa maafisa na askari ili kuhakikisha nchi inakuwa salama wakati wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *