
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) katika kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ndg. Charles Kichere pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange pamoja na Watendaji wengine wa Wizara hiyo.
Kamati za Kudumu za Bunge zinaendelea na vikao ambavyo vimeanza tangu tarehe 9 Januari 2023 na vinatarajiwa kumalizika tarehe 29 Januari, 2023 kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kumi wa Bunge.


