DKT. TULIA ATOA MSAADA WA BIMA ZA AFYA BURE KWA WANANCHI WAKE MBEYA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa niaba ya taasisi ya Tulia Trust ametoa msaada wa bima za afya 3000 bure kwa Wananchi wa Jimbo hilo ambapo wanufaika wakuu wakiwa ni Wazee, Walemavu na Wenye uhitaji maalum (wasiojiweza)

Katika hafla hiyo iliyofanyika leo Januari 24, 2023 katika ukumbi wa Tughimbe Jijini humo, Pamoja na mambo mengine Dkt. Tulia pia amewawezesha mitaji ya biashara wakinamama watano ambao kila mmoja amempatia Shilingi 200,000 ambapo jumla kuu ikiwa ni Shilingi 1,000,000 ili waweze kujiongezea kipato na kuendesha familia zao.

Katika hatua nyingine, Dkt. Tulia ametoa msaada wa viti mwendo viwili kwa walemavu wa viungo lakini pia ametoa msaada wa miwani kwa wagonjwa wa macho 159 ambao walifanyiwa upasuaji katika zoezi la huduma ya upimaji macho iliyofanyika mwezi Disemba 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *