BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA KUSUKWA UPYA.

OR-TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange (Mb) amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI imeanza kufanya marekekebisho na Maboresho ya Muundo wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa ili kuipa nguvu na uwezo wa kutoa Mikopo yenye tija na kufuatilia Marejesho.

Ameeleza hayo Januari 23, 2023 wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya USEMI ikipokea na kujadili taarifa ya Utendaji wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa na taarifa ya utendaji wa Shirika la Masoko ya Kariakoo kwa mwaka wa fedha 2021/23.

“Ni kweli Bodi ya Mikopo imekuwa na Sheria za zamani, kwahiyo tunaboresha sheria na kanuni kwa kuweka miongozo itakayosaidia bodi ya Mikopo kuwa na Uwezo wa kutoa Mikopo na kufuatilia Marejesho” ameeleza Dkt. Dugange

Dkt. Dugange amesema Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa itaongezewa nguvu ili kuiwezesha kuwa na Majukumu ambayo yako wazi ambapo yatazisaidia halmashauri kunufaika na Mikopo.

Amesema moja ya jukumu msingi la Bodi hiyo ni kuzikopesha Mamlaka za Serikali za mitaa kwa madhumuni ya kutekeleza miradi iliyolenga kuziongezea mapato, kuchochea shughuli za kiuchumi, kuongeza ajira na kuboesha utoaji wa huduma.

Wakati akijibu hoja zilizojitokeza kuhusu Utendaji wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Dkt. Dudange amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI tayari imetoa maelekezo kwa Makatibu Tawala Mikoa kuhusu utaratibu na viwango vya kufuata wakati wa kujenga masoko ili kuepuka na kupambana na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakitokea.

Aidha, Dkt. Dugange amesema ili kuimarisha Usafi katika masoko, Serikali ipo mbioni kuanza utaratibu wa kubadilisha taka ngumu kuwa nishati madala ambapo Mpango huo unaendelea kufanyiwa utafiti.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za mitaa (USEMI), Mhe. Jaffari A. Chaurembo amesema Maboresho ya Muundo wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa itasaidia halmashauri kufaidika na kuipa Uwezo bodi kufuatilia Marejesho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *