IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI NA UADILIFU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) Mhe. Abdallah Chaurembo kupitia kamati yake ameipongeza Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kwa usimamizi mzuri na uadilifu katika matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo walizotengewa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2021, ambapo idara hiyo imeokoa kiasi cha shilingi milioni 800 ambazo zimeelekezwa katika maeneo mengine kuwahudumia wananchi.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akichangia hoja wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Akiongoza kikao kazi cha kamati yake kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka 2021/2022, Mhe. Chaurembo amesema ni wazi kuwa, usimamizi mzuri, uadilifu na uaminifu wa watendaji wa Idara ya KumbuKumbu na Nyaraka za Taifa ndio umewezesha kuokoa shilingi milioni 800 kati ya bilioni mbili walizotengewa na Serikali.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa na baadhi ya watendaji kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

“Katika uongozi wangu nikiwa ni Mwenyekiti wa kamati hii ya USEMI, sijawahi kuona taasisi iliyoonesha uadilifu wa namna hii kwenye matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo, miradi yote iliyopangwa imetekelezwa na mmeokoa milioni 800 ambazo ni fedha nyingi,”Mhe. Chaurembo amesisitiza.

Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mhe. Chaurembo ameipongeza pia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuisimamia vema Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa iliyoweza kuwa mfano bora katika matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akiongoza kikao kazi cha kamati yake leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya USEMI ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Mhe. Pro. Palamagamba Kabudi amesema Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ni taasisi muhimu itakayoliwezesha taifa kutunza historia, urithi, tamaduni, mila na desturi zake.

Kamisha wa Maadili, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Aidha, Mhe. Prof. Kabudi ameishauri Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kutafuta na kutunza nyaraka za viongozi ambao waliwasaidia waasisi wa taifa kuijenga nchi ili vizazi vijavyo viweze kutambua na kuthamini mchango wao.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP Ibrahimu Mahumi akitambulisha watendaji alioambatana nao kwenye kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi amesema kama Sheria ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Na. 3 ya Mwaka 2002 inavyoelekeza, idara yake inaendelea kutafuta nyaraka zote muhimu zenye historia ya taifa ili kuzikusanya na kuzitunza kwa manufaa na rejea ya taifa.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makete, Mhe. Festo Sanga akichangia hoja wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Bw. Msiangi ameongeza kuwa, idara yake imekusanya nyaraka nyingi za viongozi waliowasaidia waasisi wa taifa katika kutekeleza majukumu yao na bado inaendelea na mchakato wa kuzikusanya ili historia ya taifa isipotee.  

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mhe. Mwantumu Zodo akichangia hoja wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) imepokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa pamoja na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo katika kusimamia utendaji kazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo leo jijini Dodoma kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *