SPIKA DKT. TULIA AHUTUBIA MKUTANO WA 145 WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI (IPU) NCHINI RWANDA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akihutubia katika Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Kigali (KCC) Nchini Rwanda leo Oktoba 13, 2022.

Katika Hotuba yake pamoja na masuala mengine, Dkt. Tulia amezungumzia hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kufikia usawa wa kijinsia pamoja na utayari wa Bunge la Tanzania katika kushughulikia masuala ya usawa wa kijinsia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *