RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI GEITA

Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoa wa Geita kuanzia Octoba 15 hadi Octoba 16 ,2022 na atafungua miradi mbalimbali ya maendeleo .

Akitoa taarifa hiyo Ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Martin Shigella mbele ya wandishi wa habari amesema Rais Samia Suluhu Hassan atawasili mkoani Geita tarehe 15 Octoba ,2022 kupitia wilaya ya Chato akitokea mkoani Kagera na ataelekea moja kwa moja katika Hospital ya Rufaa ya kanda ya Chato na atazindua Hospital hiyo pamoja na kuongea na wananchi wote wa Wilaya ya Chato.

Rais Samia atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wa Geita ikiwa ni pamoja na kufungua mradi wa kiwanda cha kusafisha Dhahabu Geita (Geita Gold Refinery GGR) akiwa njiani Mhe.Rais samia Suluhu Hassan atazungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Katoro na Buseresere na atapata muda wa kufanya mkutano mkubwa kwa kuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Geita katika uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita.

Kufuatia ujio wa ziara hiyo ya kwanza ya Rais Samia Suluhu Hassan Mkoani Geita toka aingie madarakani Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella amewataka wananchi wote kujitokeza na kumpokea Rais Samia mahali pote atakapo pita ikiwa ni pamoja na kumpongeza kwa kazi nzuri ambayo ameifanya katika mkoa wa Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *