
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Umri chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls) inaendelea na mazoezi ya Mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini India.
Mazoezi hayo yamefanyika asubuhi ya Oktoba 13, 2022 katika fukwe za Hoteli walipofikia wachezaji hao, ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Ufaransa Oktoba 15, 2022 Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru jijini Goa India.
Katika mechi ya awali iliyochezwa Oktoba 12, 2022 kati ya Ufaransa na Canada, timu hizo zilitoka sare ya Goli 1 – 1.
