RC SHIGELLA AMTAKA MKURUGENZI GEITA KUREJESHA VITABU VYA GUEST HOUSE KABLA YA SAA TISA JIONI.

Mkuu wa Mkoa Wa Geita Mhe.Martin Shigella amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Kurejesha mara moja vitabu vya kusaini wageni ambao hulala kwenye nyumba hizo (GUEST HOUSE) kabla ya kufika saa tisa jioni, ikiwa ni baada ya vitabu hivyo kuchukuliwa pasi na maelezo yeyote kwa wamiliki wa vyumba hivyo Mjini Geita.

Ametoa agizo hilo ikiwa ni kufuatia Malalamiko ya umoja wa wamiliki wa vyumba vya kulaza wageni (GUEST HOUSE) zaidi ya 90 Mjini Geita kukutana Octoba 12 na kukubaliana ifikapo tarehe 15 Octoba 2022 kama bado hawajarejeshewa vitabu vyao basi watafunga kwa kusitisha kutoa huduma ya kulaza wageni mpaka uongozi wa juu utakapo ingilia kati .

Mwenyekiti wa Umoja wa wamiliki wa vyumba vya kulala Wageni Mjini Geita Selemani Maganga amesema kitendo kilichofanywa na Afisa biashara pamoja na Mkureugenzi wa Halmashauri ni kitendo ambacho hakikubaliki kwa sababu ya kukosa maelezo ya kutosha juu ya kunyang’anywa vitabu vyao na kila mara walipojaribu kuona uongozi huo uliwakimbiza kwa kudai wanataka faini ya shilingi laki tatu.

Hata hivyo Wamiliki wa vyumba vya kulala wageni wamedai wapo tayari kutoa kodi kama serikali inavyo elekeza kwa manufaa ya taifa, huku wakisisitiza kupewa elimu ya kutosha juu ya ulipaji wa kodi kwani mpaka sasa hawana elimu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *