UVCCM MBEYA MJINI YAMPONGEZA SPIKA DKT. TULIA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM jimbo la Mbeya Mjini Clemence James Mwandemba amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa maendeleo unaoendelea jijini humo ikiwa ni pamoja na miundombinu bora.
Pongezi hizo amezitoa leo jijini Dodoma wakati akizungumza na Uhondo Media ambapo ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Akson ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa bega kwa bega na jimbo lake katika shughuli za kimaendeleo na utekelezaji mzuri jimboni mwao na Tanzania kwa ujumla.


Aidha Mwenyekiti huyo, akizungumza kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Mbeya Mjini amempongeza Spika wa Bunge Dkt. Tulia kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kundi la Kanda Ya Afrika Ya Umoja Wa Wabunge Duniani (IPU), kwani ameipa heshima nchi ya Tanzania na Afrika huku akielekeza ushauri wake kwa vijana kuchangamkia fursa hiyo Kimataifa.
“Spika wetu wa Bunge la Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia ambaye ni Mbunge wetu ameipa heshima Tanzania na Afrika na bado anazidi kuongeza tabasamu kwa Watanzania, lakini piah hatutamuacha nyuma Rais wetu, Rais wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, sisi kama vijana tutazidi kutoa ushirikiano kwani ametuletea miradi ya maendeleo” Alisema Clemence James Mwandemba.


Amesema kutokana na kazi nzuri ya Dkt. Tulia inayoonekana kwa Taifa ni kutokana na ujasiri wake, lakini piah ni mchapakazi na mwepesi kutatua changamoto za wananchi kwani amezidi kuongeza tabasamu kwa Wanambeya, hivyo wao kama vijana wanafarijika kwa kuwa atazidi kufungua fursa kwa vijana hapa nchini.
“Pia ni Mchapakazi na jasiri ambaye anatatua changamoto za wananchi wake na Mpaka sasa tunaona anaendelea kuleta fursa hapa nchini na vijana wapaswa kuchangamkia fursa hiyo” Alisema Clemence James Mwandemba .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *