UJENZI WA JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA NDEGE CHA SONGWE WAFIKIA ASILIMIA 68.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akimsikiliza Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Eng. Danstan Komba kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la abiria katika kiwanja hicho wakati Waziri huyo alipokagua maendeleo yake Mkoani Mbeya.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akikagua kazi za uwekaji ngazi za kwenye jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe. Mkoani Mbeya.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Eng. Danstan Komba (mwenye reflector) na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Eng. Matari Masige mara baada ya kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la abiria katika kiwanja hicho Mkoani Mbeya.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe ambapo hadi sasa umefikia asilimia 68. Jengo hilo litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 600 kwa wakati mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *