Wachimbaji wadogo wa Madini ya Dhahabu Mkoa wa Geita [GEREMA] wameahidi kuachana na kutumia Imani za kishirikina katika shughuli zao za uchimbaji wa madini kufuatia kupata elimu ya kutoka katika maonesho ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya madini Mkoa wa Geita ambayo yaliyomalizika Octoba 8,2022.

Akizungumza na Uhondo Tv Katibu Mkuu wa Chama Cha Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Geita Jacob Bongo amesema kwa sasa wamebadilika kwa kiasi kikubwa baada ya kuendelea kupewa elimu zaidi na kuwasaidia wachimbaji wengi kuachana na Imani za kishirikina katika kazi zao za uchimbaji wa Madini.
Katika maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini Waziri wa Madini Mhe.Dkt.Dotto Biteko aliwataka wachimbaji wadogo kuanza kufanya shughuli zao za uchimbaji wa kisasa kwa kutumia teknolojia ambayo ni bora na kuacha kuchimba kizamani kwani, ulimwengu huu umekuwa wa kisasa huku akisisitiza wachimbaji hao kuacha utoroshaji wa madini kwani serikali imeshaafanya mabadiliko ya sheria kwa kufuta kodi ambazo zilikuwa ni kero kwao na badala yake waende kuuza dhahabu zao katika masomo maalumu yaliyotengwa na kutoa onyo kali kwa wale wote ambao wanashusha thamani ya madini nchini kuanza kusakwa huku akitaja kuwa baadhi yao wameshakamatwa na muda wote wote watafikishwa mahakamani.
