WAZAZI WAOMBWA KUWAPA MALEZI BORA WATOTO WAO

Wazazi na Walezi Mkoani Geita wameombwa kuwapa malezi bora na kuwalinda watoto wao walio hitimu elimu yao ya msingi kwa mwaka huu 2022 wakati wakisubiria matokeo yao kutangazwa na kujiunga na kidato cha kwanza .

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale  Mhe.Jamhuri William katika mahafari ya darasa la saba katika shule ya sekondari ya Royal Family iliyopo mkoani Geita akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Wa Geita Mhe.Martin Shigella kwa kuwataka wazazi kuwa mstali wa mbele kwa kuhakikisha kila mzazi na mlezi anatimiza majukumu yake katika kumlinda mtoto na kuhakikisha watoto wote watakao chaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaripoti shuleni mapema kwa sababu serikali imeweka mazingira mazuri ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na madarasa ya kutosha pamoja na elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita.

Mkurugenzi wa Shule ya Royal Family Msingi na Sekondari Mhandisi Lazaro Philipo amesema shule hiyo imekuwa ikitoa malezi bora kwa kila mwanafunzi kwa kipindi chote ambacho watoto hao wanapokuwa shuleni hapo kwa lengo la kutengeneza jamii yenye maadili na kizazi bora kijacho ambacho kimekulia katika malezi yaliyo bora hata hivyo shule ya Royal family primary school imeendelea kufanya vizuri katika matokeo yake ya mitihani ya kitaifa. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *