SPIKA DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA MABUNGE RWANDA

Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha Kundi la Mabunge ya Afrika katika Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali (KCC) Nchini Rwanda.

Dhima kuu ya Kikao hiki ni kupata muunganiko wa mambo ya ujumla yanayohusu Afrika na kupata nafasi ya kuyasogeza kwenye Mkutano Mkuu wa 145 unaotarajiwa kuanza rasmi kesho trh 11 Oktoba 2022, KCC Kigali Rwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *