RAIS MWINYI AANZA ZIARA YA SIKU NNE CHINI OMAN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Ali Mwinyi, asubuhi ya leo Jumanne tarehe 11 Oktoba ameondoka Zanzibar kuelekea Oman kwa ziara ya kikazi ya siku nne kufuatia mwaliko wa Mfalme wa nchi hiyo.

Rais Dk Hussein Ali Mwinyi, katika ziara hiyo ameambatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi, baadhi ya Mawaziri na wakuu wa idara na mashirika mbalimbali ya Serikali na wafanyabiashara.Katika uwanja wa ndege wa Sheikh Abeid Amani Karume, Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi aliagwa na Makamu wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdullah, viongozi mbalimbali wa vya siasa, Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama wa SMZ na SMT.

Akiwa nchini Oman Dk. Mwinyi atakutana na Mfalme wa Oman, Sultan Haitham bin Tariq, Wafanyabiashara, Wana-Diaspora na atatembelea miradi mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *