
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akishiriki Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali (KCC) nchini Rwanda.
Dhima kuu ya mkutano huo ni kujadili “Usawa wa Kijinsia na Mabunge yanayozingatia masuala ya kijinsia kama vichocheo vya ustahimilivu na amani Duniani” ulioanza leo Oktoba 10, 2022.
Mhe. Spika ameambatana na Wabunge Wawakilishi kwenye Umoja huo ambao ni Mhe. Joseph Mhagama, Mhe. Elibariki Kingu, Mhe. Esther Matiko, Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ulenge, Mhe. Ramadhan Ramadhan pamoja na Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa J. Mwihambi, ndc.



