
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema lengo la kuundwa kwa kikosi kazi cha wajumbe 11 ambacho kitafanyakazi ya kuchambua maoni ya masuala ya demokrasia na kuhakikisha Zanzibar inaendesha shughuli za kisiasa kwa hali ya amani, umoja na mshikamano.
Ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar baada ya uzinduzi na utambulisho wa kikosi kazi hicho.
Baada ya kuhutubia wajumbe wa kikosi kazi hicho Rais Dk.Mwinyi amemkabidhi taarifa itakayosaidia wajumbe hao Mwenyekiti wa kikosi hicho Dkt. Ali Uki.




