CHAMA CHA ACT WAZALENDO WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JUMUIYA YA WANAHABARI WA MITANDAO YA KIJAMII (JUMIKITA)

Chama cha ACT WAZALENDO kupitia Ofisi ya Wasemaji wa Kisekta wamepata fursa ya kutembelea Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) kwa lengo la kuboreha ushirikiano na vyombo vya habari.

Akizungumza na Wanahabari Waziri Mkuu Kilivuli kukoka ACT WAZALENDO, Ndugu Dorothy Semu amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuweka mfumo wa kuboresha mitaji ya Wanahabari wa Mitandaoni ili kuiwezesha sekta hiyo kukua na kuweza kupata vifaa vya kisasa ili kuweza kuongeza wigo wa ajira kwa vijana.

Pia amegusia suala la uhuru wa vyombo vya habari na kuitaka Serikali kuweka sheria rafiki na sheria wezeshi ili sisiweze kuvikandamiza vyombo vya habari ambavyo ni muhimu katika jamii ya watanzania.

Aidha Naibu msemaji wa sekta ya Afya kutoka ACT WAZALENDO ndugu Rukaiya, ameongeza kuwa Serikali inatakiwa kuchukuwa shida za wananchi kama shida zake katika mradi wa bima za Afya na kuishauri Serikali iweze kuchakua changamoto za Shirika la Bima la Taifa NHIF huku akigusia sababu zilizo pelekea kufilisika kwa Shirika hilo kuwa ni Changamoto ya utawala bora, mfumo bora wa kugharamia shirika hilo, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na uwepo wa vituo vichache vya utoaji wa huduma ya Afya.

ACT WAZALENDO Wameitaka Serikali kuweza kuongeza kasi ya utoaji wa huduma ya Afya ili kuweza kuwasaidia wananchi wa hali ya chini na kusaidia familia kuweza kumudu gharama za Afya bila kuwepo kwa matabaka.

Ziara ya ACT WAZALENDO bado inaendelea katika Vyombo Mbalimbali vya habari ili kuweza kuboresha mahusiano kati ya Wanahabari na Chama hicho.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *