MIRADI 76 YA UTALII NA UTAMADUNI IMEANZISHWA NCHINI -MHE. PINDI CHANA

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema jumla ya miradi 76
ya Utalii wa Utamaduni imeanzishwa katika Kanda za Kaskazini, Kusini na Kanda ya
Ziwa ambazo zinaendelea kutangaza nchi ya Tanzania.
Amesema hayo Oktoba 07, 2022 jijini Arusha wakati akitoa salamu za wizara yake
katika Uzinduzi wa Tamasha la Maasai Festival litakalofanyika mwaka 2023, ambapo
mgeni rasmi katika hafla hiyo alikua Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Pauline Gekul.
“Wizara imetenga eneo la Makumbusho lililopo Dar es Salaam kwa ajili ya kutangaza
Utalii wa Utamaduni ikiwemo Mila, Desturi, vyakula, na mavazi” amesema Mhe. Chana.
Mhe. Chana ameongeza kuwa, Maasai Festival ni Moja ya mazao ya Utalii wa
Utamaduni ambayo yatasaidia kutangaza nchi vyema na kuongeza Idadi ya watalii
kutembelea vivutio vya nchi na kuongeza pato la Taifa.
Tamasha hilo ni miongoni mwa matamasha ambayo yanafanyika nchini kwa lengo wa
kuhamasisha, kutangaza na kurithisha Utamaduni wa Watanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *