WAZIRI KAIRUKI AKABIDHIWA OFISI NA WAZIRI BASHUNGWA

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah J. Kairuki amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Innocent L. Bashungwa ambaye sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Hafla hiyo ya makabudhiano imefanyika Makao Makuu wa Wizara yaliyopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma Leo tarehe 06 Oktoba 2022.

Makabidhiano hayo yamefanyika kufuatia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kumteua Mhe. Angellah J. Kairuki kuwa Mbunge na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na kumteua Mhe. Innocent L. Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *