HEKAHEKA ZA 16 BORA SHIMIWI ZAPAMBA MOTO

Na Mwandishi Wetu-Tanga

Ni siku ya Sita ya mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) Oktoba 6, 2022 yanaendelea jijini Tanga huku viwanja vya michezo mbalimbali vikiwa na heka heka za timu kusaka ushindi ili kujiweka kwenye hatua nzuri ya kufuzu kuendelea hatua ya 16 bora ya mashindano hayo inatarajiwa kuanza Oktoba 9, 2022 jijini Tanga.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bi Emma Lyimo ameshuhudia timu ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inavyoendelea kutoa dozi katika mchezo wa netiboli kwa timu pinzani wanapokutana nazo katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea jijini Tanga.

Leo Oktoba 6, 2022 imekuwa wakati mzuri wa kupata ushindi mnono kwa kuichapa timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika viwanja vya Bandari jijini Tanga kwa kuwafunga kwa jumla ya magoli 23-4 huku mashabiki wa timu hiyo wakiwa wenye furaha na bashasha kwa ushindi wa timu yao inayoendelea kujikusanyia alama na kujihakikishia kusonga mbele kwa hatua ya timu 16 bora ambayo inatarajiwa kurindima Oktoba 9, 2022 jijini Tanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *