WAZIRI MCHENGERWA ATEMBELEA KLABU YA FENERBEHCHE

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametembelea moja ya klabu kongwe na mashuhuri duniani, Fenerbehche ya Uturuki, na kukubaliana kushirikiana katika maeneo ya mafunzo, kambi na ujenzi wa shule za michezo.

Akizungumza katika kikao kilichoongozwa na Mjumbe wa Bodi ya Klabu hiyo anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Bw. Bekir Irdem, Waziri Mchengerwa pia ameishukuru klabu hiyo kwa kuwahi kuwa na mchezaji kutoka Tanzania, Mbwana Sammatta, na kuikaribisha klabu hiyo kuja kuweka kambi ya msimu mpya mwakani nchini Tanzania.

“Leo tu badae tutakuwa na kikao cha Bodi na nitawasilisha mapendekezo haya ili tuweze kuanza ushirikiano wetu mara moja,” aliahidi Bw. Irdem.

Katika ziara hiyo Mhe. Mchengerwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Lt. General Yacoub Mohammed na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *