TIMU YA KUVUTA KAMBA YA TAMISEMI YASHINDA SHIMIWI

Asila Twaha, Tanga

TIMU ya wanawake ya Kuvuta Kamba ya TAMISEMI imeibuka na ushindi wa pointi 2-0 dhidi ya timu ya MSD katika michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali(SHIMIWI).

Ushindi wa TAMISEMI katika mchezo huo uliofanyika leo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara umeifanya timu hiyo kuendelea na mechi ya michezo hiyo.

Akizungunza mara baada ya ushindi huo, Katibu wa timu ya TAMISEMI, Bw. Alex Morice ameushukuru uongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuendelea kuwaamini na kuendeleza ushirikiano kwa timu hiyo.

Pia ametoa wito kwa timu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo na hatimaye kutwaa ubingwa.

Naye Kocha wa timu ya kuvuta kamba ya TAMISEMI, Bw. Chediel Masinga ameipongeza timu yake kwa ushindi walioupata na kuahidi kuendelea kufanya vizuri.

“ Wachezaji wengi wa timu hii ni wapya lakini kutokana na kusikiliza maelekezo na kujituma wameweza kufanya vizuri na ninaamini tutafanya vizuri katika michezo ijayo na hatimaye kutwaa ubingwa” amesema Chediel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *