SERIKALI KURUDISHA UTAMADUNI WA KUTAZAMA FILAMU KATIKA KUMBI ZA SINEMA.

SERIKALI kupitia Bodi ya filamu Tanzania imesema ina mpango wa kurudisha utamaduni wa kutazama filamu katika Kumbi za Sinema itakayorudisha hadhi ya michezo ya kuigiza hatua inatarajiwa pia kutoa mchango stahiki katika uchumi wa wadau wa Sekta na Taifa kupitia viingilio vya mlangoni.

Aidha Bodi hiyo imepanga kuanzisha filamu za Kimkakati zitakazo saidia kutunza kumbukumbu za kihistoria kwa kuhusisha taarifa za viongozi mbalimbali waliofanya mambo makubwa kama vile Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye alisaidia ukombozi wa nchi mbalimbali barani Afrika.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma leo,Oktoba 4 na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo wakati akilezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Bodi ya Filamu pamoja na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na kueleza kuwa
Program hiyo ina lengo la kuratibu uandaaji wa filamu zenye maudhui ya kutangaza utajiri wa nchi katika eneo la utamaduni, historia na jiografia.

Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kujenga mapenzi hasa kwa vijana wa kitanzania kwa nchi yao kwa kuwaongezea ufahamu wa rasilimali waliyonayo.

Akizungumzia fursa za Ajira ya filamu nchini alisema kwa kipindi cha Januari hadi Disemba, 2021 pekee inakadiriwa kuwa ilichangia takriban ajira 30,000 zilizotokana na Filamu (waigizaji, waandaaji na watoa huduma) ambapo kwa mazingira ya Kitanzania, Filamu moja (wastani wa watu 20, tamthilya moja wastani wa watu 100) kiasi ambacho ni ongezeko la nafasi 5,000 kutoka 25,000 kiasi kinachokadiriwa kuzalishwa mwaka 2020.

“Katika uratibu wa matukio ya Tasnia mwaka 2021 Serikali ilifanya TAMASHA LA TUZO ZA FILAMU ambalo kilele chake kilifanyika jijini Mbeya Tarehe 18 Disemba, 2021 na kutunuku Tuzo na zawadi kwa watu 30 waliofanya vizuri zaidi katika vipengele mbalimbali kwenye eneo la Filamu ambapo mwaka huu Tamasha hilo linatarajia kuzinduliwa na Waziri mwenye dhamana mwezi huu wa Oktoba na kufikia kilele chake mwezi Disemba, 2022,”amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *