
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg. KENANI KIHONGOSI kwenye mkutano na waandishi wa habari iliyofanyika leo Makao Makuu ya UVCCM Taifa Dodoma ametoa taarifa kwa waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa nafasi mbalimbali ngazi ya Taifa kuwa wanatakiwa kufuata ratiba ya usahili kama ifuatavyo;
“Tarehe 08/10/2022, wagombea nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa. Tarehe 9/10/2022 wagombea wote wa nafasi ya Ujumbe wa Baraza Kuu Viti vitano, wajumbe wa kuwakilisha Jumuiya za Chama UWT na Wazazi.Tarehe 11/10/2022 wagombea wa Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa viti vitano.”
“Wagombea waliogombea nafasi mbalimbali mbali ngazi ya taifa watatakiwa wafike makao makuu Dodoma kwa usahili wakiwa na nyaraka zao kama zilivyo ainishwa katika fomu zao kwa maana ya Cheti cha kuzaliwa, Kadi za unachama CCM & UVCCM, Vyeti vya masomo au mafunzo na, Kadi ya NIDA au namba za NIDA.”
Alihitimisha kwa kusema kuwa muda wa vikao hivyo ni saa Mbili kamili asubuhi (2:00).